1 Nyakati 1 (NEN)

Kumbukumbu za historia kuanzia Adamu hadi Abrahamu
(Mwa 5:1‑32; 10:1‑32; 11:10‑26)
Adamu hadi wana wa Nuhu
1 Adamu, Sethi, Enoshi,
2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
3 Henoko, Methusela, Lameki,
Nuhu.
4 Wana wa Nuhu walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi.
Wana wa Yafethi
5Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
6Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
7Wana wa Yavani walikuwa:
Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
Wana wa Hamu
8 Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misri1:8 yaani Misraimu, Putu na Kanaani.
9Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
10 Kushi akamzaa
Nimrodi, ambaye alikua shujaa mwenye nguvu duniani.
11Misri akawazaa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 12Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
13Wana wa Kanaani walikuwa:
Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, 14Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15Wahivi, Waarki, Wasini, 16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Wana wa Shemu
17 Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mashi1:17 yaani Mesheki.
18Arfaksadi akamzaa Shela,
Shela akamzaa Eberi.
19Eberi alipata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi1:19 maana yake Mgawanyiko, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
20Wana wa Yoktani walikuwa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21Hadoramu, Uzali, Dikla, 22Obali, Abimaeli, Sheba, 23Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.
24 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,
25 Eberi, Pelegi, Reu,
26Serugi, Nahori, Tera,
27 Tera akamzaa Abramu (yaani Abrahamu).
Jamaa ya Abrahamu
28 Abrahamu alikuwa na wana wawili: Isaka na Ishmaeli.
Wazao wa Hajiri
(Mwa 25:12‑16)
29 Hawa ndio wazao wao:
Ishmaeli akazaa Nebayothi mzaliwa wa kwanza; kisha Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31Yeturi, Nafishi na Kedema.
Hao ndio wana wa Ishmaeli.
Wazao wa Ketura
32 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:
Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
Wana wa Yokshani walikuwa:
Sheba na Dedani.
33Wana wa Midiani walikuwa:
Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.
Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.
Wazao wa Sara
34 Abrahamu alikuwa baba wa Isaka.
Wana wa Isaka walikuwa:
Esau na Israeli.
Wana wa Esau
(Mwa 36:1‑19)
35 Wana wa Esau walikuwa:
Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
36 Wana wa Elifazi walikuwa:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;
Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
37 Wana wa Reueli walikuwa:
Nahathi, Zera, Shama na Miza.
Watu wa Seiri waliokuwa Edomu
(Mwa 36:20‑30)
38 Wana wa Seiri walikuwa:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
39 Wana wa Lotani walikuwa wawili:
Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
40 Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aya na Ana.
41 Mwana wa Ana alikuwa:
Dishoni.
Nao wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
42Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
Watawala wa Edomu
(Mwa 36:31‑43)
43 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:
Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 51Naye Hadadi pia akafa.
Wakuu wa Edomu walikuwa:
Timna, Alva, Yethethi, 52Oholibama, Ela, Pinoni, 53Kenazi, Temani, Mibsari, 54Magdieli na Iramu.
Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.