Zaburi 134 (NEN)
Zaburi 134
Wito wa kumsifu Mungu
Wimbo wa kwenda juu.
1 Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana,
ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.
2 Inueni mikono yenu katika patakatifu
na kumsifu Bwana.
3 Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia,
awabariki kutoka Sayuni.