Zaburi 149 (NEN)
Zaburi 149
Wimbo wa kumsifu Mungu kwa wema wake
1 Msifuni Bwana.149:1 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 149:9.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
2 Israeli na washangilie katika Muumba wao,
watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza
na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
4 Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake,
anawavika wanyenyekevu taji la wokovu.
5 Watakatifu washangilie katika heshima hii,
na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.
6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao
na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
7ili walipize mataifa kisasi
na adhabu juu ya mataifa,
8wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
wakuu wao kwa pingu za chuma,
9 ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.
Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.
Msifuni Bwana.